RUBY ADAIWA KUWA NA KIBURI

0

Msanii mwenye sauti ya ninga kutoka nchini Tanzania Ruby anadaiwa kuwa na kiburi.

Madai haya yametolewa na msanii mwenzake katika kundi la THT kwa jina Max Spesho.

Kulingana na Spesho, Ruby hua ana madharau na majivuno, jambo linalofanya kuwa vigumu kwa wasanii wengine kufanya naye kazi.

Madai haya kuhusu Ruby yanachipuka baada ya Ruby kukataa kufanya show iliyoandaliwa na kituo kimoja maarufu cha Radio nchini Tz Fiesta, akidai hakuridhishwa na malipo aliyokua anapewa licha ya kutia saini mkataba wa kufanya show.

Itakumbukwa kwamba Ruby alikosekana katika video ya wimbo kwa jina “Su” alofanya na Yamoto Band huku madai yakitolewa kwamba alikwepa kimaksudi kufanya video ya wimbo huo.

Je yanayosemwa ni ya kweli? Mda ndio utakao toa jibu.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar