MSANII HUYU AKIRI KWENDA KWA WAGANGA.

0

Msanii anaae chipukia kwa sasa nchini Tanzania kwa jina Galatone, amekiri mbele ya umma kwamba amewahi i kwenda kwa wa Waganga wengi wa kienyeji ili afanikiwe kwenye sanaa ya muziki.

Galatone ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake “Samaki”anasema ilifika wakatia katika safari yake ya kimziki alichoka kuuhangaikia muziki na ikamlazimu kutafuta usaidizi kutoka kwa nguvu za giza.

“Nimefanya sana nimeenda kwa Waganga maana kuna kipindi nilichoka kabisa nkasema acha nikajaribu, nshavunja nazi, kuchinja kuku na kila kitu yani ili tu nitoboe kwenye game,” alisema.

Hata hviyo Galatone amekiri kuwa hakupata chochote na wala hakuona mabadiliko yoyote na akaamua kuachana na mambo hayo na kumtegemeea mungu tu.

Je unadhani nguvu za kiza zina uwezo wa kumfanya msanii kufaulu kimziki?

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar