MADEE ATAMANI KUWATAJA VIGOGO WA MADAWA YA KULEVYA

0

Mwanamuziki kutoka kundi la Tip Top Connection, Madee, amedai kuwa kama angekuwa anatumia madawa ya kulevya na tayari ameshaathirika na madawa hayo asingesita kuwataja wauzaji wote wa dawa hizo.

Madee anadai kufanya hivyo kungeisadia serikali ya tz katika kupambana na vita ya uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya ambao unawathiri sana vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa hilo.

“Ningekuwa mimi natumia madawa ya kulevya na yameshaniathiri ningesema ilikuwaje hadi nikaanza kutumia dawa hizo, nimenunua kwa nani, na yule aliyeniuzia angesema anayemuuzia hadi kwa kigogo ambaye ndiye mwenye biashara yake,” alisema Madee

Ameongeza kuwa ingawa wasanii wana nafasi yao katika kupambana na biashara ya madawa ya kulevya, serikali ya taifa hilo ndio chombo ambacho kinaweza kupambana na biashara hiyo na kuitokomeza kabisa.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

RAPPER FABOLOUS AUMBUKA, MESSAGE ZAKE ZAANIKWA

Rapper maarufu kutoka nchini Marekani Fabolous amejipata akiogolewa aibu baada ya mrembo aliyekua akimtongoza katika mtandao wa kijamii kuanika message zake mitandaoni. Fiorella Zelaya ameweka ...
Skip to toolbar