LINAH AKOMA KUANIKA WAPENZI WAKE. JE KWA NINI?

0

Nimekoma! Hili ni jibu la Linah kwa swala la kumuanika mpenzi wake kwa mashabiki katika tasnia yamziki wa kizazi kipya.

Linah anasema amekoma kuwaanika wapenzi wake kwani amegundua hiyp ndiyo sababu hupelekea yeyey kutodumu nao.

Linah amefichua kuwa amekuwa akijiuliza sababu ya kutodumu na wapenzi wake na akagundua ile tabia ya kujiposti kimahaba na wapenzi wake ndiyo chanzo.

“Huwa sipendi kuwa na mtu kisha nikaachana naye, hasa yule ambaye moyo wangu umemkubali, lakini ilikuwa kila ninayeingia naye kwenye uhusiano, nikishaanza tu kumuanika huanza kujitokeza mambo ya kutuachanisha.

“Wengine ndipo wanapopata nafasi ya kuniharibia kwa kumpelekea vijineno na mwishowe tunaachana,” alisema Linah ambaye mara ya mwisho alikuwa akitoka na jamaa aitwaye William Bugeme.

Je unachukuliaje swala la kuanika mpenzi wako kwa marafiki na umma kwa ujumla?

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

EDDY KENZO ASEMA HAOGOPI MUSEVENI

Msanii wa mziki nchini Uganda Idrisa Musuuza aka Eddy Kenzo, amesema haogopi kusema ukweli kuwa wananchi ndio wenye nguvu kushinda serikali. Katika interview moja ya ...
Skip to toolbar