KALA JEREMIAH AFICHUA SABABU YA WASANII WENGI KUTOIMBA NYIMBO ZA UJUMBE

0

Msanii wa Hip hop nchini Tanzania Kala Jeremiah anadai kuwa vyombo vya habari vimechangia kwa kiasi kikubwa wasanii wa Bongo Fleva kuacha kuimba nyimbo zenye ujumbe kama ilivyokuwa zamani.

Kala Jeremiah anadai kuwa vitu vingi vya radio vinaendeshwa kibiashara zaidi kuliko kuangalia maisha kitu ambacho yeye anaona si sawa kwani vyombo vya habari vina jukumu la kuelimisha pia.

“Wasanii wengi siku hawatoi nyimbo zenye ujumbe mzito kwa sababu promotion ya nyimbo kama hizo sio kubwa, yaani hazizunguki sana.

kala-jeremiah

Kala Jeremiah amepiga mfano wa msanii mkongwe Ferooz aliyerudi katika game majuzi kupitia kibao chake kipya kwa jina ”Nimejifunza.”

“Mfano Ferouz angetoa wimbo wake wa ‘starehe’ kipindi hiki asingepata air time kwa sababu tu mtu wa radio angeona kupiga wimbo huo ni kufanya tangazo la ukimwi kitu” ameeleza Kala.

Je unakubaliana na kala jeremiah kwamba vituo vya radio vnachangia wasanii wasiku hizi kutoimba nyimbo zenye ujumbe?

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

DEMARCO AJIANDIKIA MISTARI YA KISWAHILI

Msanii Arrow Boy amekataa madai kwamba alimuandikia mistari ya Kiswahili msanii Demarco raia wa Jamaica katika collabo yao ya wimbo “Love Doctor” Akizungumzia collabo hiyo, ...
Skip to toolbar