JOSE MOURINHO ATOA MAONI YAKE KUHUSU LIONEL MESSI. JE KASEMA NINI?

0

Kocha Jose Mourinho hivi karibuni amefanya mahojiano na kimoja cha Televisheni na kutoa maoni yake juu ya kukutana na Lionel Messi kama mpinzani hasa kwenye michuano ya Champions League.

“Messi amewahi kushinda Champions League na makocha tofauti. Nadhani ni rahisi kushinda ukiwa nae kuliko ukicheza dhidi yake” Mourinho amesema.

Kocha huyo Mreno bado anaamini kwamba kucheza kwa mfumo wa “teamwork” ni muhimu katika kupata ushindi.

“Mimi ni kocha wa timu ya soka. Najua kwamba wakati mwingine watu wanadhani kwamba mchezaji mmoja mmoja ni muhimu kuliko timu. Bado nafikiri kwamba timu ni muhimu zaidi kuliko chochote. Lakini ni ukweli dhahiri kwamba kuna baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kufanya tofauti,” alisema.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

DIAMOND APATA KIMWANA KIPYA. NI MKENYA!

Msanii Diamond Platnumz wa nchini Uganda amezua gumzo jipya mitandaoni baada ya kufichua kuwa kapata mchumba mpya. Kupitia kaunti yake ya instagram, Diamond ametaja mwanadada mmoja ...
Skip to toolbar