HII NI REKODI NYINGINE ALIYOVUNJA DRAKE NA ALBUM YAKE “VIEWS”

0

Drake ameendelea kuvunja rekodi na album yake inayokimbiza kwenye chart mbalimbali duniani ya “Views” iliyotoka tarehe 29 April mwaka huu.

YMCMB wametangaza kuwa nyimbo za album hiyo zimesikilizwa zaidi ya mara Billion 1 kwenye mitanadao nchini Marekani pekee ndani ya wiki tatu za mwanzo tangu iachiwe.

Album hiyo imeshika namba moja kwenye chart ya Billboard 200 kwa wiki tano mfululizo huku wimbo wa One Dance aliomshirikisha Wizkid na Kayla ukiendelea kushika namba moja kwenye chart ya Billboard Hot 100 tangu uachiwe.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar