DON JAZZY ATOA SABABU ZA KUPUNGUA KWA COLLABO ZA WANIGERIA NA WAMAREKANI.

0

Producer Mnigeria Micheal Collins Ajereh aka Don Jazzy amefichua sababu inayopelekea kupungua kwa kolabo za wasanii wa Nigeria na wale wa Marekani, licha ya mataifa haya mawili kutawala mziki wa kisasa ulimwenguni.

Don Jazzy anasema sababu kuu ni hatua ya wasanii wa Marekani kubadilisha muziki wao ili ulingane na ule unaovuma kwa sana barani Afrika.

don jazzy2

Don Jazzy  anasema baadhi ya wasanii wa Marekani waliomuita kufanya naye kazi baadae huogopa sababu hawako tayari kubadilisha muziki wao.

“Wasanii wengi Marekani wameniita na nimetengeneza kazi zao ili ziwe kwenye sound itakayopenya Afrika ila wakiisikia huwa wanataka uibadilishe tena mpaka iwe ya kimarekani sababu hawako tayari kubadilisha muziki wao, ni waoga, ndio maana collabo za Wamarekani na sisi zitakuwa chache sana“.

Don Jazzy aliwahi kuwa studio wakati inatayarishwa album ya Beyonce na kwa sasa msanii wake Tiwa Savage yupo Roc Nation ya Jay Z.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar