CHRIS BROWN ASHINDA KESI

0

Chris Brown ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili kuhusu malezi mabovu ya mtoto wake iliyofunguliwa na mzazi mwenzake Nia Guzman.

Mzazi mwenzake Nia Guzman alifika mahakami akidai kuwa Chris hana malezi sahihi na muongozo unaostahili juu ya mtoto wao Royalty akitaka apokonywe haki za kumlea mtoto.

Chris-Brown-baby-is-named-Royalty

Bi.Guzman alidai Chris amekuwa akivuta sigara na bangi yeye na marafiki zake mbele ya mtoto wao na imempelekea Royalty kupata maradhi ya pumu.

Katika maamuzi ya kesi hii katika mahakama ya Califonia jaji aliruhusu malezi sawa kutoka kwa wazazi wote wawili  ambapo sasa Chris Brown anaruhusiwa kuspend siku 12 na mtoto wake kila mwezi bila masharti yoyote.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar