BURNA BOY ATANGAZA KUSTAAFU MZIKI.

0

Msanii wa miondoko ya Dancehall kutoka nchini Nigeria Burna Boy amewashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza kustaafu mziki.

Kupitia akaunti yake ya Twitter,  Burna Boy amesema kuwa ataacha muziki baada ya tamasha lake litakalofanyika mjini London October 1.

Hata hivyo wapo mashabiki wengine waliojitokeza na kumkejeli Burna Boy kuwa anatafuta kiki zisizo na mpango ili tu kuipromote show yake ya London, jambo lililoonekana kumkasirisha Burnaboy.

download (14)

Vile vile Mwimbaji wa kimataifa kutoka Uingereza Lily Allen ambaye alitarajiwa kutoa naye collabo amejitokeza na kumshtumu Burna Boy na kumkumbusha kuhusu kolabo yao.

Muda mfupi baadaye Burna Boy aliwapunguza kidogo presha mashabiki zake kuhusu mustakabali wake wa kustaafu kwa mfululizo wa tweets wenye ujumbe unaoashiria kughairi tangazo lake.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

JE BELLE 9 ANAHAMIA WASAFI (WCB)?

Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii mwengine wa wa R&B nchini humo Belle 9 akasaini ndani ya label hiyo pia. ...
Skip to toolbar