BABA AMUUA MWANAWE  KWA KUANGUKA MTIHANI

0

Mwanamume mmoja anazuiliwa na polisi nchini Japan baada ya kumuua mwanawe wa miaka 12 kwa  ku’ fail mtihani wa shule.

Kulinga na taarifa hizi, Kengo Satake mwenye umri wa miaka 48, amemuua mwanawe kwa kumdunga kisu.

Inasemekana awali kabla ya kisa hicho, baba aligombana na mwanawe kuhusiana na swala la kutojitayarisha kwa mtihani ambao ungemwezesha kujiunga na shule moja ya kifahari iwapo angeupita.

middle lined up 1

Inadaiwa ushindani katika kujiunga na shule za kifahari Japan umeongezeka, ambapo wazazi hufanya kila wawezalo kuhakikisha watoto wao wanajiunga shule hizi, ambazo mara nyingi hua kama hakikisho kwa maisha bora ya baadae kwa watoto wao.

Mtoto huyo kwa jina Ryota alifikishwa hospitali moja akiwa na jeraha la kuchomwa kisu kifuani, lakini alifariki baada ya kupoteza damu nyingi na babke alinaswa na polisi baada ya madaktari kuripoti kifo cha mtoto.

Baba wa mtoto amekiri kumchoma kisu lakini akajitetea kwamba ilikua bahati mbaya

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

RAPPER FABOLOUS AUMBUKA, MESSAGE ZAKE ZAANIKWA

Rapper maarufu kutoka nchini Marekani Fabolous amejipata akiogolewa aibu baada ya mrembo aliyekua akimtongoza katika mtandao wa kijamii kuanika message zake mitandaoni. Fiorella Zelaya ameweka ...
Skip to toolbar