BAADA YA RICH MAVOKO, MSANII MWENGINE AMEZEA MATE KUFANYA KAZI WCB

0

Baada ya Rich Mavoko kujiunga rasmi na kambi ya Wasafi, msanii Abdul Kiba ameweka wazi kwamba  yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani.

Ni wazi kwamba tetesi za uwepo wa bifu kati ya Ali Kiba na Diamond unathiri mpaka wasanii wengine  wa karibu  wanaowazunguka wasanii hawa.

IMG-20150406-WA0001

Hata hivyo Abdu Kiba amabaye ni kaka wa Ali Kiba, amesema kuwa kama WCB  itakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri yeye binafsi anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo.

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar