ALI KIBA AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA

0

Mwanamuziki wa Tanzania, anayetamba na wimbo wake mpya ‘Lupela’, ameendelea kuwaacha njia panda mashabiki wake baada ya kudai kuwa yeye na mrembo Jokate Mwegelo, ni marafiki licha ya kudaiwa kuwa ni wapenzi.

Kwa muda mrefu Ali Kiba na Jokate, wameonekana kuwa na urafiki wa karibu sana na watu wengi kuhusisha urafiki wao kuwa ni wa kimapenzi, japokuwa mara kadhaa wamekuwa wakikanusha na kudai wao ni marafiki.

 

DIAMOND589

Akihojiwa Ali Kiba, amedai kuwa ni vigumu kuachana na rafiki ila ni rahisi kuachana na mpenzi na kusisitiza kuwa siku hizi watu wanasahau kuwa wazee wa zamani walikuwa wanachagua vipi wasichana kwani siku hizi watu wanaoana tu.

Amedai kuwa mtu anaweza kuishi na mpenzi wake kwa muda mrefu hata miaka mitatu, lakini ni vigumu kuachana na rafiki.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar