MZIKI WA SINGELI WATISHIA BONGO FLEVA Tz

0

Kwa kasi inayokua mziki wa Singeli nchini Tanzania kwa sasa ni wazi kwamba unauwezo wa kuupoteza mziki wa Bongo Fleva.

Staa wa mziki huo wa kitmaduni nchini Tz Amani Hamisi jina maarufu ‘Man Fongo’ amewatahadharisha wasanii wa bongo flavaz kwamba wasipochunga huenda mashabiki wa mziki wa Bongo flavaz wakahamia mziki wa singeli sababu sasa ndio unaopeta Zaidi mitaani.

man fongo @ mtiwadawa

Man Fongo ambaye amepachikwa jina la Mfalme wa Singeli, kwa sasa anasumbua na kibao chake cha kwa jina Hainaga Ushemeji ambacho nitakuchezea katika mda mfupi.

Man Fongo anasema wasanii wa Bongo Fleva wanakazi kubwa kuhakikisha wanabaki kileleni kutokana na namna muziki wa Singeli ulivyopokelewa vizuri na mashabiki mitaani.

“Ujue wao wanaimba vitu vya kubuni wakati sisi tunaimba maisha halisi hasa ya uswahilini kwa masikini wenzetu,” anasema Man Fongo.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar