WHATSAPP INAPATIKANA KWA LUGHA YA KISWAHILI.

0

Baada ya mitandao ya kijamii maarufu duniani kama Twitter na  Facebook kuitambua lugha ya Kiswahili na kuiingiza rasmi kwenye App zao,  mtandao wa kijamii wa WhatsApp nao rasmi umeingiza lugha hiyo kwenye App yake.

Kuanzia sasa watumiaji wote duniani wanaovutiwa na Lugha ya Kiswahili watakuwa na uwezo wa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye App hiyo yenye watumiaji zaidi ya watu bilioni 1 duniani kote.

Mabadiliko hayo ni hatua kubwa kwa lugha ya kiswahili na huenda ikachangia mitandao mingine mikubwa kama Instagram kutambua lugha ya kiswahili kwenye App zao.

Jinsi ya kubadili lugha WhatsApp na kuweka kiswahili

Hatua ya kwanza hakikisha ume-update WhatsApp yako kisha nenda kitufe cha Settings kisha bonyeza Chats na select App Language utakutana na Lugha mbili Kiswahili na Kiingereza na uchague Kiswahili. Tayari utakuwa umepata WhatsApp yako kwa lugha ya kiswahili.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar