WASHAMBULIWA KWA  KU-COPY & PASTE WIMBO.

0

Kundi moja maarufu la muziki nchini Rwanda kwa jina  Dream Boyz  limejikuta likishambuliwa na wadau wa muziki wakiwemo mashabiki wao nchini humo baada ya ku-copy & paste wimbo ‘SIKINAI’ wa msanii Beka Flavour wa nchini Tanzania.

Wadau walianza kuliandama kundi hilo kwenye mtandao wa YouTube baada ya video ya kuachilia video ya wimbo huo kwa jina Romeo & Julieth wiki iliyopita.

Wadau wengi waliosikiliza ngoma hiyo wametoa maoni kuwa kitendo hicho si cha kiungwana na kinarudisha nyuma maendeleo ya muziki wa Rwanda.

Wimbo huo mpaka sasa tayari umetazamwa zaidi ya mara laki moja katika kipindi cha wiki moja tangu utoke.

Hata hivyo kundi hilo bado halijazungumza chochote kuhusu tuhuma hizo.

Kwa upande wake Beka Flavour yeye amepokea  taarifa hizo na kuuliza mashabiki wake alifanye nini kundi hili.

 

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar