VITUO 23 VYA RADIO VYAFUNGWA UGANDA.

0

Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imetangaza kuvifungia vituo 23 vya redio kwa kurusha matangazo ya waganga wa kienyeji.

Katika mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa tume ya mawasiliano Uganda Godfrey Mutabazi amevishutumu vituo husika kwa kile alichokitaja kama kuwaruhusu waganga wa kienyeji kutangaza matangazo yao na kuvunja sheria kuhusu uchawi nchini humo.

Radio hizo zimekuwa zikiwapa vipindi waganga hao wa kienyeji kutangaza uganga wao, huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kwa njia ya simu.

Tume hiyo imedai baadhi ya waganga walikua wakiwarai waskilizaji kutuma hela kuptia simu na keshoye wangejipatia mamilioni ya fedha  chini ya kitanda chao.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

RAY C MWIZI WA BWANA?

Msanii wa kike kutoka Tanzanian Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C, anadaiwa kuiba mume wa wenyewe. Mwezi uliopita, Ray C alitupia picha mtandaoni ...
Skip to toolbar