UTAFITI: WANAUME WENYE NDEVU NYINGI NI “HUSBAND MATERIAL”.

0

Utafiti mpya wa kisayansi sasa umebaini kuwa wanaume wenye ndevu huwavutia zaidi jinsia ya kike katika swala la mapenzi.

Katika utafiti ulifanywa na Barnaby Dixson katika kitivo cha saikologia katika chuo kikuu cha Queensland nchini Australia, wanawake huhusisha ndevu nyingi katika uso wa mwanamume na uwezo wake wa kuwa bwana mzuri katika ndoa.

Utafiti huu ambao tayari umechapishwa rasmi katika jarida la ufahamu wa kisayansi la Evolutionary Biology, ulihusisha wanawake 8,520, ambapo walionyeshwa picha za sura tofauti za wanaume na kuulizwa kuchagua wanaume wanaodhani ni wazuri katika maswala ya ndoa.

Wanawake wote waliwachagua wanaume wenye ndevu nyingi usoni kama ‘husband material” huku waliokua na ndevu chache ama kukosa ndevu kabisa, wakitajwa kama wanaume wanofaa kwa mahusiano ya mda mfupi na wala si ndoa.

Comments

comments

Our Rating

0
Reader Rating: (0 Rates)
0

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar