UTAFITI MPYA: KUTUMIA VYOMBO VYA PLASTIKI KULIA CHAKULA KUNASABABISHA MAGONJWA HAYA KWA BINADAMU.

0

Usitumie  kabisa vyombo vya plastiki kuchemshia au kuwekea vyakula vya moto kama chai, maziwa, supu, maji, ugali n.k.

Wataalamu wa afya wametoa ripoti ya utafiti mpya ambayo umethibitisha  kwamba, plastiki inapopata moto huzalisha kemikali iitwayo BPA (Bisphenol A) ambayo ikiingia mwilini husababisha magonjwa mengi kwa binadamu.

Miongoni mwa magonjwa  yaliotajwa kutakana na kutumia vyombo vya plastiki ni pamoja na magonjwa ya ini, magonjwa hatari ya moyo,kisukari, magonjwa ya kizazi kwa jinsia zote, kuathirika kwa nguvu za kiume, pumu huongezeka kwa wagonjwa wa pumu, huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha kupoteza kumbukumbu.

KUMBUKA

Madhara ya plastiki huonekana baada ya muda mrefu ambapo unaweza kuvitumia vyombo hivyo na kutoona madhara yake katika muda mfupi lakini baada ya miaka ipatayo kumi utapata ugonjwa ambao utashindwa kujua chanzo chake.

TAHADHARI

Hakikisha huweki vyakula vya moto kwenye vyombo vya plastiki nyumbani kwako na badala yake tumia vyombo vya udongo au glasi,au bati.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar