USHER RAYMOND AMLIPA EX WAKE BAADA YA KUMWAMBUKIZA UGONJWA WA ZINAA.

0

Msanii wa RnB Usher amemlipa fidia Ex wake baada ya kumuambukiza ugonjwa wa zinaa miaka kadha iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa za mitandaoni nchini Marekani, Usher ametoa dola milioni 1.1 kumaliza kesi iliyomkabili toka mwaka 2012.

Kulingana na makaratasi ya kortini yaliyopatikana, Usher Raymond alipatwa na ugonjwa aina ya Malengelenge ambao kwa kizungu hujulikana kama Herpes kati ya mwaka 2009 na 2010 na kumuambukiza binti moja kimakusudi.

Usher aliomba msamaha baada ya tukio hilo lakni alifunguliwa kesi jijini Los Angeles sababu ni sheria kwenye mji huo kama una ugonjwa wa zinaa ni lazima kumfahamisha mpenzi wako.

Usher alitoa dola milioni moja na laki moja kumaliza kesi hii mnamo Dec. 28, 2012.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar