UHASAMA BAINA BEBE COOL NA A PASS WAPAMBA BURUDANI UGANDA

0

Msanii mkubwa nchini Uganda A Pass ameendeleza uhasama wake na msanii mwenza Bebe Cool nchini Uganda.

Kwa kejeli, A Pass jana ametangaza kumzawadi yeyote atakaye mripoti mtu aliyetengeneza na kusambaza picha mtandaoni inayomuonyesha Bebe Cool akiwa nguruwe.

A Pass na Bebe Cool wamekua katika mgogoro wa maneno karibuni baada ya Bebe Cool kununua mbuzi na kumwita A Pass.

A Pass hakufurahishwa na kauli ya bebe cool baada ya picha kadhaa zinazomuonyesha akiwa kama mbuzi kuanza kusambaa mitandaoni.

Haijajulikana nani alitengeza picha ya Bebe Cool akiwa nguruwe, lakini imesambaa siku chache baada ya inayomuonyesha A Pass akiwa kama mbuzi.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar