TOTTENHAM HOTSPURS YALAZWA NYUMBANI – UEFA

0

Klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza jana ilipoteza mechi yake ya kwanza ya kuwania kombe la UEFA, baada ya kulazwa nyumbani na klabu ya AS Monaco ya Ufaransa, katika mechi iliyosakatwa katika uwanja wa Wembley.

Wageni Monaco waliichapa Tottenham Hotspurs mbele ya mashabiki wake jumla ya mabao 2 – 1 katika mechi ya kundi “E”.

As Monaco ilipata mabao yake kupitia wachezaji Bernardo Silva na Thomas Lemar, huku Tottenham ikipata bao lake la kufutia machozi kupitia mchezaji Toby Alderweireld.

Katika mechi nyengine ya kundi “E” iliyosakatwa jana,

Klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani imetoka sare ya mabao 2 – 2 na klabu ya CSKA Moscow ya Urusi.

Kwa sasa As Monaco ya Ufaransa imechukua uongozi wa kundi E ikiwana alama 3, CSKA Moscow ni ya pili na alama moja, Bayer Leverkusen ya Ujerumanini ya tatu na alama moja pia huku Tottenham ikivuta mkia bila alama.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar