SUGU ATANGAZA RASMI KUSTAAFU MUZIKI

0

Msanii mkongwe wa Hip Hop hapa Tanzania, Joseph Mbilinyi aka Sugu ametangaza rasmi kustaafu muziki.

Kupitia maelezo aliyo’post katika  akaunti ya mtandao wa instagram Sugu amesema kwa sasa atajikita kwenye majukumu mengine.

Sugu amesema kuwa anaamini ameutoa mbali muziki wa Hip Hop Tanzania, na anajiandaa kuangalia namna ya kustaafu kwa kuwaachia mashabiki wake zawadi ya mwisho.

Hata hivyo Sugu hakuweka bayaa zawadi gani ataachia mashabiki wake kuwaaga rasmi kati ya kuwaachia album ya mwisho ama kuwaandalia concert.

Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ni moja ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop ambao walianza muziki miaka ya 1990’s na kwa sasa ni mbunge katika bunge la Tanzania akiwakilisha eneo la  Mbeya

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar