STANTMASTAZ YAJIBU MADAI KUHUSU AMARILA

0

Baada ya msanii Amarila kubadili management yake na kujiunga na Hustle Nation, iliyokua management na studio yake Stantmastaz imejitokeza kupinga uvumi kwamba hatua ya Amarila ilichochewa na ulegevu wa studio hiyo katika safari yake ya kimziki.

Majuzi taarifa za msanii Amarila kuhama Stantamastaz zilipoanza kusambaa, Stantamstza ilituma ujumbe wa kupongeza uamuzi wa Amarila na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mapya huku ikijivunia kuafikia lengo lake la kulea kipaji chake hadi kilipoonekana na Hustle Nation.

Hata hivyo, baadaye madai yalisambaa kwamba hatua ya Amarila imesababishwa na kuchoka na hatua ya Stantmastaz kutomshughulikia kimziki.

Stantmastaz imejitokeza kueleza kuwa ilichokifanya kufika sasa ni ndio uliokua uwezo wake na kutaja hatua ya Amarila kuwa mwanafunzi wa sekondari kama mojawapo ya vizingiti na changamoto iliyokua ikizuia Stantmastaz kuongeza kasi ya safari yake ya kimziki.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

PROFESA JAY ATANGAZA HILI

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Morogoro na rapa nguli nchini Tz, Joseph Haule ‘Prof Jay’ amesema licha ya kuwa na wadhifa wa ubunge, bado ataendele ...
Skip to toolbar