SIZE 8 ALAZIMIKA KUJIELEZA KWA MASHABIKI.

0

Mwimbaji wa nyimbo za injili jijini Nairobi Size 8 amejipata katika wakati mgumu baada ya mashabiki katika mitndao ya kijamii kumtaka kueleza kwa nini siku hizi havai tena pete yake ya ndoa.

Size 8 ambaye alifunga ndoa na Dj mmoja maarufu katika ulimwengu wa Gospel Music DJ MO, karibuni amevumishwa kutalikiana na mumewe, huku ikiripotiwa kuwa tayari kaihama nyumba yao ya ndoa.

Hata hivyo, Size 8 ambaye amezaa na DJ MO mtoto mmoja wa kike, amejitokeza kuupinga uvumi huu na kuwakashifu wote wanao-usambaza uvumi, akidai wanamuombea mabaya.

Size 8 ameeleza kwamba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita amekua havai pete yake ya harusi sababu haimtoshi tena, baada ya kuongeza uzito wa mwili.

Size 8 ameongeza kuwa kwa sasa yupo katika mpango wa mazoezi kila siku ili kupunguza mwili wake.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar