SASA NI RASMI.DIAMOND KUFUNGA NDOA 2019 TAREHE HII!

0

Msanii DiamondPlatnumz kutoka Tanzania amethibitisha kwamba ako katika mipango ya kufunga ndoa na mpenzi wake mpya raia wa Kenya, Tanasha Donna Oketch.

Diamond amefichua kuwa ndoa hiyo itafungwa mwaka ujao 2019, Februari tarehe 14, ambayo kawaida hua siku ya wapendanao aka Valentines Days.

Diamond ameeleza kuwa ameamua kuoa na kutulia ili apate mda murua wa kushughulikia biashara zake nyingi, akihoji kuwa anahitaji mwanamke ambaye atamsaidia katika kusimamia biahsra zake zote akijipanga kwa maisha ya kesho.

Diamond kwa sasa anamiliki biashara za kituo cha TV na Radio, Digital Platform, Diamond Karanga na RecordLabel ya Wasafi.

Hata hivyo, tangazo lake limezua gumzo mitandaoni kwani tarehe aliyoichagua ni siku sawia na tarehe ambapo aliyekua mpenzi wake Zari The Boss Lady, alitangaza rasmi kuachana na Diamond Platnmuz mapema mwaka huu.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar