Msanii mkubwa wa muziki Tanzania, Ali Kiba amelazimka kuifuta video yake mpya ya wimbo kwa jina “Hela” katika mtandao wa YouTube, baada ya kushambuliwa na mashabiki.
Inasadikika kuwa King Kiba ameufuta wimbo masaa machache baada ya kuuweka, kutokana na mapokezi mabaya aliyoyapata kwenye mitandao ya kijamii.
Wengi wamechukizwa na hatua kwamba wimbo “Hela” ulitoka mwaka wa 2015 na badala ya kutoa kazi mpya kama wasanii wengine, Ali Kiba ameamua kutoa video yake miaka mitatu baadaye.
Aidha viwango vya video hiyo vimekashfiwa ikisemekana haviendani na hadhi yake kama msanii mkubwa, pamoja na matarajio ya soko la mziki kwa sasa.
No comments