ROMA AZUNGUMZIA TETESI KZA KUMCHANA BABU TALE.

0

“….Boss amemganda Dangote, ameisahau Tip Top….”

Huu ni mstari unaopatikana katika wimbo mpya wa Roma alioshirikisha Darasa na Jos Mtambo. Mstari huu unaendelea kuzua mshawasha miongoni mwa wakereketwa wa taarifa za burudani afrika mashariki.

Katika mitandao ya kijamii baadhi wanadai kuwa Roma amemponda Babu Tale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Diamond na pia ni meneja wa kundi la Tip Top.

roma

Hata hivyo Roma amejitokeza kuzungumzia mstari huu.

Roma anasema kuwa hakumaanisha kumponda meneja huyo kama watu wengi wanavyodhani bali alitaka kufikisha ujumbe kuwa watu wasisahau walipotoka lakini kwa njia ya kisanii zaidi.

“Tafsiri ya mstari huo ni kwamba tusisahau tulipotoka,ningeweza tu kuandika hivyo lakini kama msanii inabidi niwe mbunifu,ndio nikajenga hiyo picha na ndiyo maana watu wameukumbuka zaidi” Roma alifafanua.

Unakubaliana na maelezo ya Roma kuhusu mstari huu?

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar