REUBEN KIGAME AFICHUA SIRI YA KUTUNGA NYIMBO ZA KUDUMU.

0

Kawaida nyimbo za wasanii wa kizazai kipya hupoteza umaarufu wake na kusahaulika miongoni mwa mashabiki baada ya kipindi kifupi nyingi ikiwa  takribani miaka miwili hivi.

Je, umewahi kujiuliza labda nini kinachopelekea hali hii?

Msanii mkongwe wa nyimbo za injili Reuben Kigame ameelezea kitu anachoona kinasababisha nyimbo za wasanii wengi wa kikazi kipya kuchujuka kwa haraka.

Kigame anasema wasanii wasikuhizi wanaimba nyimbo zakusifia vitu visivyodumu milele kama mapenzi na starehe.

Akipiga mfano nyimbo za tenzi za roho katika dini ya kikristo, kigame anasema mtu anapoimba kuhusu mwenyezi mungu bilashaka wimbo utadumu kwani vitu vyote duniani vitapita isipokua neno la mungu.

Kigame amepiga mfano wa nyimbo za injili za wasanii marehemu kama Angela Chibalonza ambazo bado zinawakosha mioyo baadhi ya wasikiliazji wa nyimbo za injili hadi sasa.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar