RAY C MWIZI WA BWANA?

0

Msanii wa kike kutoka Tanzanian Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C, anadaiwa kuiba mume wa wenyewe.

Mwezi uliopita, Ray C alitupia picha mtandaoni akiwa na jombi mmoja mwenye asili ya kizungu katika pozi la mahaba alipokua katika ziara ya kimziki nchini Uingereza.

Sasa mwanadada mmoja raia wa Kenya anayeishi Uingereza kwa jina Doky, amejitokeza mitandaoni na kumkashifu Ray C kwa kile anachodai kama kumuibia bwana, baada ya Ray C kuhamia na kuanza kuishi katika nyumba ya jombi huyu nchini Uingereza.

Doky ameeleza kuwa jombi, ambaye anaonekana katika picha ya Ray C alikua mchumba wake waliyekua tayari wameshavishana picha ya uchumba wakijitayarisha kwa ndoa, lakini alibadilika punde baada ya kupatana na msanii Ray C.

Doky pia ame post picha za kimahaba akiwa na jombi anayepiganiwa kuthibitisha madai yake ya uchumba na mzungu huyo.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar