RAPA NIKKI MBISHI AMCHANA BABU TALE

0

Rapa Nikki Mbishi amefunguka na kusema kuwa meneja wa wasanii Babu Tale ni mmoja kati ya watu wana ua talanta za wasanii Bongo.

Kpita mistari yake aliyopost katika mtandao wa kijamii, Nikki amedai babu tale ni tataizo ambalo hata rais Magufuli na waziri wake hataweza kulitataua.

Nikki Mbishi amesema anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Babu Talent’ ambao mashairi yake yanaonekana kumchana meneja wa kundi la Tip Top Connection na kudai kuwa meneja huyo ni jipu, na halitaweza kutumbuliwa katika awamu ya tano ya Rais Magufuli.

Naitwa Babu talent a.k.a jipu ambalo Magufuli na Nape Nnauye hawataliona mpaka wanamaliza uongozi wao” alindika Nikki Mbishi.

Katika baadhi ya mistari ya Nikki Mbishi inaonesha kuwa Babu Talent ndiyo chanzo cha baadhi ya wasanii kupotea kimuziki licha ya wasanii hao kuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye muziki.

Ningekuwa na roho nyepesi ningeshavuta unga, Babu Talent nishampoteza hadi Daz Baba siyo kama siyo mkali ila nimeamua tu” aliandika Niki Mbishi .

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar