RAPA FABULOUS AEPUKA KIFUNGO JELA.

0

Msanii maarufu nchini marekani Fabulous ameepuka kifungo cha hadi miaka 20 jela, baada ya kuingia katika makubaliano na kiongozi wa mashtaka katika kesi ya kujeruhi mtu inayohusisha mchumba wake.

Kulingana na taarifa kutoka Bergen County, jimbo la New Jersey, rapa Fabulous amekubali kuanza mpango maaulum wa kubadili tabia unaopewa watuhumiwa waliofanya makosa kwa mara ya kwanza ili waepuka adhabu ya mahakama iwapo kesi itaamuliwa.

Mnamo Oktoba mwaka jana, Fabulous alifunguliwa mashtaka ya kushambulia na kumjeruhi mchumba wake aliyezaa naye watoto 2 kwa jina Emily Bustamante baada ya kukosana.

Fabulous na Emily Bustamante kwa sasa wamerudiana na wanaishi pamoja.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

AUDIO || BOB T – ACHA IKAE

<<DOWNLOAD/LISTEN NEW AUDIO HIT>>  ARTIST : Jaykah Mtengwa & Mchafuzy –  Mbona Mapema: Kujipakulia nyimbo mpya za wasanii wengine kutoka kanda ya pwani.Tembelea HULKSHARE: Teddy Mwanamgambo HEARTHIS: Teddy ...
Skip to toolbar