RAIS UHURU KENYATTA AMUOMBEA KURA MSANII. JE NI NANI?

0

Baada ya rais Uhuru Kenyatta kukamilisha kipindi kigumu cha kampeini za kisiasa, bado anaonekana ana nguvu za kuendeleza kampeini.

Rais Uhuru Kenyatta sasa anawataka wakenya kumpigia kura msanii Nyashinski katika kinyanganyiro cha tuzo za MTV EMA.

Nyashinski ameteuliwa katika kitengo cha Best African Act pamoja na wasanii wengine barani Afrika Wizkid na Davido wa Nigeria, Babes Wodumo na Nasty C wa Afrika kusini na C4 Pedro wa Angola.

Nyashinsky ana hitaji kura milioni moja kushinda kitengo hichi, ambacho kimewahi kushindwa na kundi la Saut Sol mwaka wa 2014.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar