R.KELLY ATANGAZA TOUR YA KIMZIKI BARANI ULAYA!

0

Mkongwe wa mziki wa RnB ulimwenguni kutoka nchini Marekani R. Kelly ametangaza ziara ya kimziki itakayofanyika barani ulaya katika siku zinazokuja.

Tangazo la R. Kelly linajiri wakati ambapo amezungukwa na tuhuma za kudhulumu kimapenzi wanawake katika miaka ya nyuma.

Kupitia mitandao ya kijamii, R. Kelly amefichua kuwa anapanga kwenda kutumbuiza mashabiki wake katika mataifa kama Australia, New Zealand na Ujerumani mwezi Aprili.

R. Kelly amekana madai yote aliyolimbikiziwa katika documentary “Surviving R. Kelly” iliyosambazwa mitandaoni ikionyesha mahojiano na maelezo ya namna alivyokuwa akiwanyasa kijinsia, kimwili na kiakili kwa wasichana wenye umri wa chini ya 18.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar