PESA ANAZOTAKIKANA DIAMOND KUTOA, KUPATA COLLABO NA TYGA. HUTAAMINI!

0

Msanii wa mziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platinumz amefichua kiasi cha fedha alichotakikana kumlipa msanii wa Marekani Tyga, iwapo anataka kufanya nae Collabo.

Kambi ya msanii Tyga inasemekana kutaka kulipwa dola laki moja na elfu hamsini, ambazo ni sawa na shilingi milioni 15 pesa za Kenya, kabla ya wasanii hao kuingia studio kufanya kazi ya pamoja.

 Aidha Diamond amefichua kiasi cha fedha alichotoa kupata collabo na wasanii wengine wa Marekani kama Ne-Yo na Rick Ross ambapo anadai alitoa takribani milioni 16 pesa za Kenya kufanya kazi na wasanii hawa.

Diamond amefichua haya katika kikao na halmashauri ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA, alipokua akieleza baadhi ya changamoto anazopitia ili kufanikisha kazi zake za kisanii.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar