PAPA FRANCIS AJITOSA KATIKA MTANDAO WA KIJAMII.

0

Baba Mtakatifu Fransisko amezindua akaunti mpya ya picha kwenye mtandao wa Instagram, mtandao wenye mvuto mkubwa kwa vijana wa kizazi kipya.

Inadaiwa kuwa baada ya kujiunga na mtandao  Machi 19, mwaka huu tayari Papa huyo amepata wafuasi zaidi ya milioni 1.5 wanaomfuatilia.

Akaunti yake ina jina la Franciscus, inadaiwa kuwa itamwezesha Papa Fransisko, kuwashirikisha vijana wanaojikita katika mitandao ya kijamii kuona baadhi ya picha.

Taarifa zinadai kuwa lengo ni kuvuka vikwazo vya lugha, ili kuwafikia watu wengi zaidi kwa njia ya lugha ya picha inayoweza kueleweka na watu wengi zaidi.

Baba Mtakatifu amezindua matumizi ya mtandao huu mjini Vatikani kwa kurusha picha yake ya kwanza inayomwonesha akisali.

Mtandao huu utatumika pia kuwashirikisha vijana wa kizazi kipya picha na video fupi za Baba Mtakatifu Fransisko.

Ikumbukwe kuwa Papa ana akaunti ya Twitter yenye zaidi ya watu Milioni 27 wanaomfuatilia, wakiwemo Rais wa Marekani Barack Obama na mwanamuziki Justin Bieber.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

RAPPER FABOLOUS AUMBUKA, MESSAGE ZAKE ZAANIKWA

Rapper maarufu kutoka nchini Marekani Fabolous amejipata akiogolewa aibu baada ya mrembo aliyekua akimtongoza katika mtandao wa kijamii kuanika message zake mitandaoni. Fiorella Zelaya ameweka ...
Skip to toolbar