NIKKI MBISHI MKOSOA PROFESA JAY

0

Muziki wa Singeli unaonekana kuwaumizwa vichwa wasanii wengi wa Hip Hop hasa baada ya Professor Jay kuachia wimbo wake mpya kwa jina ‘Kazi Kazi’ aliomshirikisha msanii Sholo Mwamba anayeimba mziki wa Singeli.

Profesa Jay aidha ameibandika jina kazi yao mpya na kuamua kuuita style ya “Hip Hop Singeli” jambo amabalo lilizua minong’ono miongoni mwa wanaharakati wa mziki wa HipHop bongo.

msanii wa hip hop, One The Incredible alikua wa kwanza kujitokeza na kusema kuwa hakuna kitu kama Hip Hop Singeli kama anavyodai Mkongwe wa Hip Hop ,Professor Jay.

Optimized-Prof-Jay

Jana Roma Mkatoliki alijitokeza kumteta profesa akihoji kwamba mistari ya Profesa bado ni rap licha ya kupandikizwa katika beat ya singeli.

Sasa msanii mwingine wa hip Hop, Nikk Mbishi ameendelea kusisitiza kuwa hip hop haiwezi kuchanganywa na kitu chochote.

Nikk Mbishi amemtaka Professor kusema kuwa amefanya “hip hop” na “singeli” au amefanya “Singeli” na sio “hip hop singeli” kama anavyodai kwani “Hip Hop” haichanganyiki na chochote.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar