NDOA YA BAINDO NA SHINEY YASAMBARATIKA.

0

Ndoa kati ya mtayarishaji maarufu wa mziki kanda ya pwani kwa jina Producer Baindo na msanii wa kike aliyewahi kuvuma kwa jina Shiney Ann imesambaratika.

Akithibitisha kutamatika kwa mahusiano yao, producer Baindo amefichua amekosana na shiney baadaya shiney kumshambulia baindo na kumsababishia majeraha yaliyomlazimu kupiga ripoti polisi kabla ya kuruhusiwa kupata matibabu katika hospital.

Baindo anadai kiini na shina la ugomvi wa migogoro yao ya kila mara ni ukosefu wa uaminifu upande wa Shiney ambapo amemtuhumu kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa yao.

katika ushahidi unaosambazwa na producer Baindo sauti za majibizano kati yake na shiney zipo ambapo shiney anasikika akimfyolea na kumtusi producer Baindo

Aidha zipo screenshot za jumbe za simu Baindo anazodai ni za maongezi kati ya shiney na mwanamume mmoja ambaye baindo hakumfichua.

Kwa upande wake shiney amekataa kuzungumzia taarifa hizi licha ya kupewa nafasi sawia ya kuthibitisha taarifa na kuzungumzia madai ya producer baindo dhiidi yake.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar