NAY WA MITEGO AJIBU BASATA

0

Baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuufungia wimbo mpya wa Nay wa MitegoPale Kati Patamu,’ msanii huyo amefika mahakamani kuatafuta haki.

Kulingana na Nay, hii si mara ya kwanza kwa hili kutokea, lakini safari hii ameamua kutafuta usaidiazi wa wanasheria na hatma ya wimbo huo upo mikononi mwa wanasheria wake ambao wanafuatilia haki zake kama msanii.

nay2

“Kuhusu hili suala kwa sasa mimi sina cha kuongea,nimewaachia wanasheria wangu,wao watajua nini cha kufanya. Sasa nafuatilia sheria ili nijue haki zangu, kama ni sahihi au sio sahihi ndio maana nimewachia wanasheria” alisema.

Wimbo wa Nay mpya ‘Pale Kati Patamu’ ni wimbo wa tatu kufungiwa na BASATA.

Je unadhani ni sawa wimbo wa msanii kufungiwa ikiwa unaonekana kupotosha maadili ya jamii?

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar