KING KAKA APIGA HATUA KIMATAIFA.

0

Rapa maarufu nchini mwenye makao yake jijini Nairobi King Kaka amepiga hatua kubwakatika safari yake ya kimziki, baada ya wimbo wake “Dundaing” ulipochezwa katika mechi moja ya ligi ya kikapu nchini Marekani.

Hii inajiri siku chahche baada ya hatua yake ya kuzindua album yake mpya kwa jina“Eastlando Royalty” ambayo imepokelewa vyema na mashabiki.

Katika kipande cha video alichosambaza kupitia akaunti yake ya instagramKing Kaka amejulisha mashabikiwanaomfuatilia kuwa kwa sasa mziki wake unakubalika katika soko la kimataifa.

Wimbo “Dundaing” ulichezwa wakati wa mechi baina ya  Dallas Mavericks na Portland Trail Blazers.

Itakumbukwa kwamba, KingKaka ndio msanii wa kwanza kutoka afrika mashariki na kuhojiwa katika kituo maarufu zaidi cha radio nchini Marekani, Hot97

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar