MZIKI WA AFRIKA MASHARIKI HAUCHEZWI NIGERIA – VANNESA MDEE

0

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Vanessa Mdee anadai muziki wa Afrika Mashariki haupewi nafasi kubwa nchini Nigeria, kama mziki wa Nigeria unavyopewa nafasi kanda ya Afrika Mashariki.

Vanessa ambaye yupo nchini Nigeria kutangaza albamu yake ‘Money Mondays,’ anasema nyimbo kutoka afrikamasahriki zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari nchini Nigeria ni zile ambazo wasanii wa afrika mashariki wameshirikisha wasanii wa Nigeria.

Vanessa ametaja wimbo wa Patoranking na DiamondLove You Die’ na wake kwa jina “move” alioshirikiana na msanii Reekado kama nyimbo pekee alizoskia zikichezwa nchini Nigeria.

Vanessa anadai si kwamba soko la mziki Nigeria halitambui mziki kutoka Afrika Mashariki ni mzuri, bali wa’Nigeria weneyewe waliamua kuupa kipaumbele muziki wao pekee.

Je kwa nini mziki wa Nigeria unapenya na kuskizwa sana na mashabiki wa mziki afrikamashariki?

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar