MR. SEED AIHAMA EMB RECORDS YA BAHATI.KISA?

0

Record label maarufu ya mziki jijini Nairobi kwa jina EMB (Eastland’s Most Beloved) inayomilikiwa na msanii wa injili kwa jina Bahati, imepata pigo baada ya msanii wake maarufu kwa jina Mr. Seed kutangaza kuhama EMB.

Katika tangazo lake kupitia akaunti yake ya Instagram, Mr. Seed ameeleza kuwa ameamua kuihama EMB ili kutoa nafasi kwa wasanii wengine wachanga huku akisistiza kuwa hakuna uhasama baina yake na msanii Bahati mmiliki wa record label ya EMB.

Mr. Seed ambaye amevuma na wimbo wake kwa jina “Gwara Gwara” amekuwa msanii chini ya EMB Records kwa kipindi cha miaka miwili.

Akijibu tangazo la Mr.Seed, Bahati amemtakia kila kheri Mr. Seed katika maisha yake mapya kama msanii huru.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar