MATAZAMO WA MWANAMGAMBO : Kwa Nini Baadhi Ya Nyimbo Zinakosa Nafasi Katika Radio.

0

Je, vigezo gani hutumika kuamua ni wimbo gani unapata nafasi ya kuchezwa katika kituo cha radio?

Je wakurugenzi wa mziki katika vituo vya radio huzingatia nini katika maamuzi yao kuhusu wimbo unaoingia katika playslist  za watangazaji?

MATAZAMO WA MWANAMGAMBO

Haya ni baadhi tu ya maswali mengi wasanii hujiuliza kimya kimya kila wanapofikiria kuwasilisha kazi zao mpya katika vituo ili zipate nafasi ya kusikika na mashabiki wao. Mara nyingi kufuatia ukosefu wa majibu rasmi kutoka kwa vituo na watangazaji, uzushi wa taarifa na madai yasio na ukweli hupata nafasi ya kuchipuka na mara nyingi kupelekea uhasama baina ya wasanii na wahusika katika vituo vya radio.

Leo ntajaribu kuangazia kwa kifupi vigezo ninavyoona huzingatiwa sana katika kufanya maamuzi ya nyimbo zinazopata nafasi ya kuingia katika mzunguko wa nyimbo katika kituo cha radio.

  1. Muundo Wa wimbo

Muundo wa wimbo unafaa kuwiana na mfumo ama mpangilio wa nyimbo zinazochezwa katika kituo, ukizingatia malengo ya usimamizi wa kituo husika. Vituo vya radio vimejigawanya katika mifumo tofauti inapokuja swala la mziki, kila kituo kikijaribu kulenga ama kuburudisha kundi flani la watu katika jamii. Mgawanyiko huu ndio umepeleka kuchipuka kwa vituo vinavyocheza nyimbo aina flanii pekee. Wimbo wako unafaa kuwiana na mfumo ama muundo wa kituo iwapo unataka upate nafasi ya kusikika katika kituo husika.

  1. Historia ya kimziki.

Historia yako ya kimziki katika tasnia pamoja na uhusiano wa awali na kituo hukuongezea nafasi ya wimbo wako mpya kuchezwa katika kituo. Iwapo nyimbo zako zimewahi kuchezwa katika kituo, kuna urahisi wa kazi yako mpya kukubalika kwa urahisi na kupewa nafasi sawia na nyimbo za awali. Hii ni kwa sababu watangazaji na  waskilizaji wa kituo kile wanakufahamu.

  1. Ujumbe wa wimbo wako.

Je, wimbo wako unaamsha hisia zipi katika maisha ya mskilizaji. Watangazji wengi wa vipindi sifika vya radio hupenda nyimbo zinazogusa waskilizaji kwa njia moja ama nyengine kupitia ujumbe nakadhalika. Wengi wao hucheza nyimbo wakitaka kupitisha ujumbe ama kujenga maandhari na taswira flani kwa wasikilazaji wa vipindi vyao. Ni vizuri kutathmini wimbo wako unazua msisimko gani unaposkilizwa, sababu wimbo unaosisimua zaidi na kugusa hisia unaposkilizwa na una nafasi kukukubalika na kuchezwa.

  1. Je, wimbo Unavuma?

Iwapo wimbo wako unavuma ama unanunuliwa katika soko la mziki basi bila shaka una mashabiki wengi wanaofuatilia na kupenda kazi zako. Umaarufu wa wimbo wako katika soko la kimziki unaongeza pakubwa nafasi ya kazi yako kuchezwa katika kituo vya radio.

  1. Umaarufu wako mashinani.

Umaarufu wa msanii katika eneo ambako kituo kinapepperusha matangazo yake ni jambo lenye uzito inapokuja maamuzi ya wimbo kukubalika ama kutokubalika kuingia katika mzunguko wa nyimbo za kituo. Umaarufu wa msanii katika eneo unaweza kupimwa kupitia idadi ya matamasha anayoandaa, pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wanaohudhuria. Iwapo wimbo wako unachezwa katika sehemu zengine za taifa ama vituo vyengine sawia, uwezekano wa kukubalika upo juu.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar