MAN CITY YAILAZA BORUSSIA MONCHENGLADBACH

0

Mshambulizi Sergio Aguero alifunga mabao matatu na kuisaidia klabu yake ya Manchester City ya Uingereza, kuilaza Borussia Monchengladbach ya Ujerumani mabao 4 – 0, katika mechi ya kundi  C ya kuwania kombe la UEFA iliyosakatwa jana usiku jijini Manchester

Hii ilkua mechi ya kwanza ya Manchester city chini ya mkufunzi wao mpya Pep Guardiola katika kinyanganyiro cha kombe la UEFA.

Bao lengine la Mancheste City lilipachikwa wavuni na mshambulizi Kelechi Iheanacho.

Monchengladbach ambayo ilkua inacheza ugenini, haikua na mashabiki wengi wake baada ya mechi hiyo kuahirishwa juzi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jiji la Manchester ikiandama na rad,i iliyohatarisha usalama.

Kwa sasa Barcelona ya Uhispania inaongoza kundi “C” kwa sasa ikiwa na alama tatu ikifuatiwa na Man City ya Uingereza  yenye alama 3 lakini na uchache wamabao, Borussia Monchengladbach ya Ujerumani ni ya tatu na alama 0 huku klabu ya Celtic ya Scotland ikishikilia mkia na alama 0 pia lakini imefunga mabao mengi zaidi.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

DJ PINYE AMJIBU DNA.

Baada ya msanii DNA kutoa wimbo wa kumtusi DJ maarufu nchini DJ Pinye  kufuatia uhasama uliozuka majuzi, DJ Pinyeamejitokeza kumjibu msanii DNA. Pinye amesema hababaishwi ...
Skip to toolbar