MADEE ATAMANI KUWATAJA VIGOGO WA MADAWA YA KULEVYA

0

Mwanamuziki kutoka kundi la Tip Top Connection, Madee, amedai kuwa kama angekuwa anatumia madawa ya kulevya na tayari ameshaathirika na madawa hayo asingesita kuwataja wauzaji wote wa dawa hizo.

Madee anadai kufanya hivyo kungeisadia serikali ya tz katika kupambana na vita ya uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya ambao unawathiri sana vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa hilo.

“Ningekuwa mimi natumia madawa ya kulevya na yameshaniathiri ningesema ilikuwaje hadi nikaanza kutumia dawa hizo, nimenunua kwa nani, na yule aliyeniuzia angesema anayemuuzia hadi kwa kigogo ambaye ndiye mwenye biashara yake,” alisema Madee

Ameongeza kuwa ingawa wasanii wana nafasi yao katika kupambana na biashara ya madawa ya kulevya, serikali ya taifa hilo ndio chombo ambacho kinaweza kupambana na biashara hiyo na kuitokomeza kabisa.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

AUDIO || OMMY CASSEY – MAPENZI UPOFU

<<DOWNLOAD/LISTEN NEW AUDIO HIT> ARTIST :Ommy Cassey – Mapenzi Upofu: Kujipakulia nyimbo mpya za wasanii wengine kutoka kanda ya pwani.Tembelea HULKSHARE: Teddy Mwanamgambo HEARTHIS: Teddy Mwanamgambo  JIUNGE ...
Skip to toolbar