KUCHEZA NA MCHANGA KAMA MTOTO NI DAWA YA UGONJWA HUU!

0

Kucheza na mchanga mchafu kumetajwa na wasayansi kama tiba ama njia mojwapo ya kupunguza msongo wa mawazo (stress) na kuleta afueni ya raha katika maisha ya binadamu.

Ndio! kucheza na mchnaga ama kujichafua na machanga mithili ya mtoto ni njia mojawapo ambayo imethibitishwa kisayansi kwamba inasaidia kutibu tatizo la msongo wa mawazo.

Bakteria moja kwa jina Mycobacterium Vaccae ni inayopatikana sana katika mchanga imetajwa kutibu msongo wa mawazo.

Bakteria hii imethibitishwa kuulazimisha mwili kutoa kemikali ya serotonin inayomfanya binadamu kuskia vizuri na aliyejaa furaha.

Wanasayansi wameeleza kuwa ukosefu wa kemikali ya serotonin mwilini umetajwa kuwa kiini cha tatizo la ukosefu wa raha (depression), ubababikaji (anxiety) na kukumbuka ama kujirudia kwa vitu vinavyomuogopesha ama kumpumbaza mtu.

Katika utafiti huo, bakteria hii ilidungwa panya kwa majaribio ambapo vipimo vilionyesha kuwa wanyama waliodungwa waliweza kuwa watulivu na wenye furaha.

Wanasayansi wanasema bakteria hii inaweza kuingia katika mwili wa binadamu kupitia uvutaji hewa mtu anapocheza na mchanga.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

VITUO 23 VYA RADIO VYAFUNGWA UGANDA.

Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imetangaza kuvifungia vituo 23 vya redio kwa kurusha matangazo ya waganga wa kienyeji. Katika mkutano na waandishi wa habari, ...
Skip to toolbar