KOFFI OLOMIDE AHUKUMIWA JELA MIAKA 2

0

Msanii maarufu kutoka nchini Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Congo Koffi Olomide amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono na kuhukumiwa kulipa faini ya euro 5,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi laki tano pesa za Kenya na kutumikia kifungo cha mika miwili jela iwapo atarudia kosa hili.

Wanenguaji wa wanne wa Koffi Olomide walifika mahakamani na kumfungulia mashataka wakidai kati ya mwaka 2002 na 2006, aliwanyanyasa kingono wakiwa na umri wa miaka 15 nchini Congo kabla ya kuwazuilia bila idhini yao walipohamia naye nchini Ufaransa.

oMbali na hukumu hii Olomide mwenye umri wa miak 64 kwa sasa ameamrishwa kulipa laki zengine tano pesa za Kenya kwa kosa la kuwasafirisha kinyume cha sheria wanawake watatu hadi nchini Ufaransa

Waendesha mashtaka walitaka Olomide ahukumiwe miaka saba gerezani lakini mahakama ya Ufaransa  imetupilia mbali mashtaka mengine ya unyanyasaji na madai ya utekaji nyara.

Wakili wa Olomide amekaribisha uamuzi huu na kueleza kuwa kutamatika kwa kesi hizi kutamundelea Olomide hofu ya kukamtwa anaposafiri mataifa mbali mbali.

Hii si mara ya kwanza Olomide kupatwa na mkono wa sheria kwani mwaka wa 2016 alikamatwa na kuzuliwa kwa mda aliporudi nchini kwao DRC baada ya kufurushwa nchini kwa tuhuma za kumshambulia mnenguaji wake mmoja katika uwnaja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar