KAULI YA VANESSA MDEE KUHUSU KUMWAGANA NA JUX

0

Msanii wa kike wa mziki nchini Tanzania Vanessa Mdee aka Vee Money amezungumzia tetesi zilizozagaa mitandaoni hivi punde kwamba ametemana na mpenziwe wa mda mrefu, msanii mwenza Jux.

Vanessa Mdee amepinga madai haya na kusistiza kwamba bado wapo mapenzini na msanii Jux.

Wee Money ameeleza kuwa tetesi hizi zinachipuka kutokana na kutoonekana mara kwa mara akiwa karibu na msanii Jux katika siku za hivi karibuni.

Vanessa ameeleza kuwa hilo linasababishwa na kazi zao za kimziki ambapo huhitajika kusafiri mataifa tofauti na kuwafanya kuwa mbali.

Karibuni kumezagaa tetesi kwamba wawili hawa walitengana baada ya Vanessa kumsaliti kimapenzi msanii Jux.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar