KAULI YA RICK ROSS KUHUSU MATAKWA YAKE KABLA KUJA KENYA

0

Rapa Rick Ross kutoka nchini Marekani amepinga madai kwamba ameweka matakwa ya juu kabla ya kukubali kuja Kenya kutumbuiza katika tamasha lililopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu wa April.

Kupitia twitter account yake, rapa Rick Ross amesema taarifa kwamba ameitisha vitu kama helkopta, kufungwa kwa barabara , vyumba vya hoteli za kifahari miongoni mwa matakwa mengine yasiyoeleweka ni uongo mtupu.

Jana taarifa zilisambaa kwamba Rick Ross alikataa kuja Kenya kwa tamasha hilo hadi matakwa yake yatakapotimizwa na waandalizi. Rick Ross anadaiwa kutaka;

  • Ticket 30 za ndege “first class” za wapambe wake.
  • Usafiri wa helkopta akiwasili nchini.
  • Chumba cha hoteli chenye hadhi ya presidential suite.
  • Room za 5 star hotel kwa wapambe wake atakaosafiri nao.
  • Taulo mpya 1,500.
  • Chupa 3,500 za pombe ya ghali.
  • Kufungwa kwa barabara mbili zinazoelekea uwanja wa tamasha wakati anatumbuiza.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar