KANYE WEST APEWA DAKIKA 4 TUZO ZA MTV AFANYE ATAKACHO

0

Rapa Kanye West amepewa dakika 4 kufanya atakalo, katika sherehe za utoaji tuzo za mwaka huu za MTV video awards.

Watayarishaji wa show hio mpaka sasa hawajui kama Kanye West ataamua kuzifanyia nini dakika 4 walizompa, kati ya kupiga show, kuongea au kukaa kimya tu kama kawaida yake.

Itakumbukwa kwamba kuna wakati Kanye alifanya maajabu aliposhinda tuzo, baada ya kuamua kuongea kwa jumla ya dakika 11 badala ya kufanya show kama wasanii wengine, ambapo pia alitumia mda huo kutangaza azma yake kugombania urais wa Marekani miaka ijayo.

Kanye atakuwa miongoni mwa mastaa kama  Rihanna, Future, Ariana Grande, Nicki Minaj, Britney Spears, G-Eazy, Nick Jonas na Ty Dolla $ign katika hafla hiyo.

Tuzo za video za mwaka 2016 za MTV zitafanyika New York mjini Madison Square Garden jumapili hii

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar